Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dulla Mbabe aupania ubingwa wa UBO

7965933f598523303ee9fef6a53575c2 Dulla Mbabe aupania ubingwa wa UBO

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BONDIA Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amesema kwa mawindo aliyoyaweka Kisarawe anaamini atafanya vizuri na kuchukua ubingwa wa Afrika katika pambano lijalo dhidi ya Daniel Wanyonyi kutoka Kenya.

Pambano hilo la raundi 10 la kuwania ubingwa wa Afrika wa UBO linatarajiwa kupigwa wiki ijayo mkoani Dodoma.

Akizungumza na gazeti jana Dulla alisema anafanya maandalizi mazuri akiahidi watanzania kuwa yuko tayari kupambana na kurejesha heshima yake kwa ubora atakaouonyesha.

“Nipo Kisarawe nafanya maandalizi yangu ya kutosha na kubwa najipanga kujiweka vizuri kwa ajili ya kujenga heshima, naamini mambo yatakuwa mazuri kwani mashabiki wangu hawatojutia,”alisema.

Alisema tayari amemjua mpinzani wake ni mtu wa aina gani na anamheshimu akijua mpambano hautakuwa rahisi lakini utakutanisha wapambanaji wawili wazuri.

Alisema kitakachomfanya kushinda sio tu mazoezi anayofanya bali dua pia za watanzania zitampa nguvu kubwa ya kubakiza ushindi nyumbani.

Mwishoni mwa mwaka jana bondia huyo hakuwa na matokeo mazuri katika mapambano mawili aliyocheza moja nyumbani dhidi ya Twaha Kiduku alikula kichapo na lingine alikwenda Kazakhstan na kupoteza dhidi ya bondia wa huko Bek Nurmaganbet.

Huenda hatokubali tena kupoteza mfululizo kwani kiwango chake kinaweza kushuka kama ataruhusu iwe hivyo.

Chanzo: habarileo.co.tz