Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mwakyembe ashtushwa na taarifa za Mwakinyo

Mwakyembe Mwakinyo Dkt. Mwakyembe ashtushwa na taarifa za Mwakinyo

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa zamani wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema ameshtushwa na taarifa zilizosambaa za Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo kufungiwa kucheza ngumi nchini Uingereza kwa muda usiojulikana.

Kauli hii ya Dkt. Mwakyembe imekuja baada ya Mtandao wa ngumi za kulipwa duniani (BOXREC) kuchapisha taarifa kwamba Bondia Mwakinyo amefungiwa na Bodi ya Ngumi za kulipwa Uingereza (BBBC) kushiriki pambano lolote Nchini humo.

Dkt. Mwakyembe ameandika; "Nimeshtushwa na taarifa hii ya Bondia wetu Mwakinyo kuchukuliwa hatua hiyo na BBBC, Kamisheni yetu ya Ndondi za kulipwa (PBRC) inasemaje kuhusu hili? ni kweli au ni porojo za kimtandao? kama ni kweli Kamisheni yetu imechukua hatua gani kujua sababu za hatua hiyo na kifanyike nini kumsaidia Kijana wetu ikiwa hakutendewa haki?"

Taarifa hiyo haikueleza chanzo cha Bondia huyo namba moja nchini kufungiwa ambapo hata hivyo kulingana na taratibu za ngumi za kulipwa, imeelezwa kuwa kufungiwa huko hakutoathiri yeye kucheza ngumi Nchi nyingine duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live