Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dillian Whyte, Joshua ni vita ya maneno

Skysports Anthony Joshua Dillian Whyte 4721811 Joshua na Whyte Ulingoni walipokutana

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dillian Whyte amemtaja Anthony Joshua kama mjinga namba moja akiwa anajibu kile alichokisema kuhusu pambano linalokuja la ubingwa WBC uzani mkubwa dhidi ya Tyson Fury.

Anthony Joshua alikuwa amempigia debe Whyte kuelekea pambano hilo ambalo litafanyika mwezi Aprili 23 katika uwanja wa Wembley AJ alisema: “Ninampigia debe Dillian, ingawa namchukia, na ninataka kumvunja siku moja.

Akijibu stori yake ya Instagram, Whyte alionekana kukerwa na tamko la Joshua la chuki.

Alichapisha: “Mbona uchungu sana. Mjinga namba 1. @anthonyjoshua niliwahi kukufanyia nini man.”

“Chuki ni neno kubwa nakuheshimu sana bingwa na ninataka kupigana na wewe kwa sehemu fulani.

Whyte anakumbukumbu ya kupokea kipigo cha KO katika raundi ya 7 kutoka kwa Anthony Joshua mwaka 2015.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live