Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cosmas: Adai jina la kaka yake linamtesa

11633 Pic+cosmas TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Akiwa na miaka 12, Cosmas Cheka anaanza kujifunza ngumi, wakati huo aliambatana na kaka yake, Francis Cheka ambaye hata hivyo kwa wakati huo hakuwa maarufu katika makonde.

Cosmas anasema alipenda kuambatana na kaka yake huyo ambaye amewahi kuwa bingwa wa Dunia wa WBF katika mazoezi ya ngumi na kujikuta akivutiwa kucheza masumbwi hivyo, baada ya kuhitimu darasa la saba, alijiunga na ngumi za ridhaa.

“Nikiwa kwenye ngumi za ridhaa, kaka yangu alitwaa ubingwa wa Afrika, kitendo kile kilinihamasisha na kujikuta nami nikitamani kujiunga na ngumi za kulipwa, niliongeza juhudi katika mazoezi.

“Ilipofika 2007, nilianza rasmi ngumi za kulipwa, nilifanya vile ili kufuata nyayo za Francis ambaye wakati huo hakuna bondia wa Tanzania aliyekuwa akimsumbua ulingoni,” anasema Cosmas.

Jina la Cheka limemgharimu

Cosmas ambaye amechangia baba na Cheka lakini mama zao wakiwa tofauti mara kwa mara hukutana na zomea zomea ya mashabiki wa ngumi ambao ni wapinzani wa kaka yake pale anapokuwa akipigana.

Cosmas anasema anakutana na changamoto nyingi hasa anapokuwa ulingoni anakumbana na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki ambao hawampendi kaka yake ambao ugeuzia chuki hiyo kwake huku wengi wakiamini yeye Cosmas anabebwa na jina la Cheka ingawa hana uwezo wa kupigana ngumi wakati si kweli.

“Hata nikishinda wapo wanaoona nimependelewa labda sababu ya Cheka, wengi hawapendi kuona mimi nashinda na Cheka anashinda lakini pia wapo mabondia ambao wanakamia mno wanapocheza na mimi kwa sababu tu ya jina Cheka,” anasema Cosmas.

Tofauti na wanandondi wengine, lakini Cosmas alianza kujifunza ngumi akiwa mwanafunzi wa darasa la tano shule ya Msingi Kinondoni ya Dar es Salaam katikati ya miaka ya 1990.

Chanzo: mwananchi.co.tz