Bondia Derek Chisora, ametamba kumchapa mpinzani wake Tyson Fury na kubeba taji la WBC uzito wa juu, watakapovaana kesho Jumamosi, na kusema hajali kuhusu wanaomkosoa juu ya kauli yake hiyo.
Chisora ambaye amepoteza mara 12 kwenye mapambano 45, ukijumuisha mapambano matatu kati ya manne ya mwisho, amepigwa mara mbili na Fury kabla ya pambano la kesho.
"Sijali nini kinasemwa, kwa Mimi kukata tamaa, kwa sababu tu gazeti linasema hivyo, siwezi kufanya hivyo," alisema Chisora.
Chisora mwenye umri wa miaka 38, alipigania ubingwa wa WBC miaka 10 iliyopita (Februari 2012) na kupoteza kwa pointi dhidi ya Vitali Klischko.
FURY, ndiye anayeushikilia mkanda huo wa WBC uzito wa juu tangu mwaka 2020 alipomchapa Deontay Wilder, ambapo hata hivyo miamba kadhaa ya masumbwi imeshindwa kumpora ubingwa huo.