Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cheka mdogo amshinda bondia Mmalawi

Screenshot 2020 09 14 At 09.28.15 660x400.png Cheka mdogo amshinda bondia Mmalawi

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Bondia wa Tanzania, Cosmas Cheka ameshinda pambano dhidi ya Mmalawi, Hannock Phiri lililofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Walipigana wa uzito wa Light kuwania UBO International Title ambapo pambano hilo lilikuwa la round 12. Kwa uamuzi wa majaji ameonekana kushinda japo mpinzani wake ameonekana kutokubaliana na uamuzi huo.

Mbali na hayo, Cheka amesema kuwa kama mpinzani wake hajaridhika, arudie pambano na kwamba yeye yuko tayari kumfuata Malawi.

Katika Mapambano ya utangulizi, Mwanadada Zulfa Macho, mtoto wa Yusuph Macho alishinda kwa Knock-Out kwenye round ya kwanza kwenye pambano dhidi ya Mmalawi, Ndau Chilimba.

HUYU NDIO RAIS WA MASHABIKI WA MTIBWA SUGAR TANZANIA NZIMA “ANAISHI ZANZIBAR”

Chanzo: millardayo.com