Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cheka arudi upya ulingoni, kuzichapa Aprili 28

Cheka Pic Data Cheka arudi upya ulingoni, kuzichapa Aprili 28

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADA ya kuwa nje ya ulingo kwa zaidi ya miaka miwili, Francis Cheka amerejea upya na sasa atazichapa Aprili 28 jijini Arusha.

Cheka ambaye tangu Desemba 26, 2018 alipochapwa kwa Knock Out (KO) na Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' hakuwahi kupanda ulingoni na kuhamishia makazi yake nchini Msumbiji ameanza mazoezi kujiandaa na pambano hilo.

"Nimerudi upya kwenye ngumi na naamini nitakuwa na muda mrefu zaidi wa kuonekana ulingoni," amesema Cheka.

Katika pambano hilo, Cheka atazichapa na Shaban Kaoneka bondia pekee nchini aliyewahi kumchapa Hassan Mwakinyo ingawa hivi karibuni alichapwa na Suleiman Kidunda kwenye ukumbi wa Mlimani City.

"Kaoneka si bondia wa kumbeza, ana rekodi na historia nzuri kwenye ngumi za kulipwa, nimeanza mazoezi kuhakikisha nafanya vizuri na ninarudi upya kwenye ngumi.

"Mashabiki wangu wamekuwa wakinihoji ni kwanini sirudi ulingoni, niliamua kukaa kando na kujipanga upya, lakini sasa narudi kwa nguvu mpya," anasema Cheka ambaye sasa atakuwa akipigania uzani wa light heavy.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz