Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changarawe, Chala kupanda ulingoni leo

Chala Changarawe, Chala kupanda ulingoni leo

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabondia wawili wa timu ya Taifa ya Ngumi "Faru Weusi wa Ngorongoro" Nahodha Yusuf Changarawe na Azizi Chala leo watapanda ulingoni kwa nyakati tofauti katika hatua za nusu fainali katika mashindano ya Mandela Cup yanayoendelea nchini Afrika Kusini. - Changarawe aliyeshinda juzi kwa mara ya pili dhidi ya mpinzani wake mkubwa katika bara la Afrika Orabi Abdelgawwad Salah kutoka Misri, anatarajiwa kupanda ulingoni kupambana na Phillipus Tangein kutoka Namibia katika uzani wa Light Heavyweight kilo 80. - Changarawe atapambana kutokea kona ya Blue katika Session ya kuanzia majira ya saa 9 mchana muda wa Tanzania. - Wakati huohuo bondia mwingine chipukizi na toleo jipya katika kikosi hicho Azizi Chala, akishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kimataifa atapambana dhidi ya Trofimus Johannes kutoka Namibia. - Chala atacheza kutokea upande mwekundu katika Session ya pili ya jioni itakayoanza kuanzia majira ya saa moja usiku muda wa Tanzania. - Mashindano haya mapya ya Mandela yaliyoasisiwa na Raisi wa Shirikisho la Ngumi la Dunia IBA Umar Kremlev na kuandaliwa na IBA kwa kushirikiana na Shirikisho la Ngumi Afrika (AFBC) na Shirikisho la Ngumi la Afrika ya Kusini (SANABO) yalianza rasmi Aprili15,2024 na yatafikia tamati kesho Jumapili kwa michezo ya fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live