Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changalawe atinga Nusu Fainal All African Games

Yusuf Changalawe.jpeg Bondia wa Tanzania, Yussuf Changalawe

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa Tanzania, Yussuf Changalawe amefanikiwa kutinga Nusu Fainali katika Mchezo ya Afrika (All African Game) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda Maxinillano Bibano wa Equatorial Guinea uzito wa Light Heavy kufuatia Refa Kusimamisha Pambano (RSC) Raundi ya kwanza tu kumnusuru na kipigo zaidi mpinzani ukumbi wa Bukom Arena Jijini Accra.

Kwa ushindi huo, Changalawe ambaye ni Nahodha wa timu hiyo ya taifa ya ndondi inayojulikana kama Faru Weusi wa Ngorongoro amejihakikishia kushinda Medali kwenye michezo ya Mwaka huu nchini Ghana na sasa atakutana na Pita Kabeji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Nusu Fainali.

Mabondia wengine wa Tanzania waliotinga Nusu Fainali na kujihakikishia Medali ni Ezra Paul Mwanjwango uzito wa Light na waliofanya hivyo ni Musa Maregesi uzito wa Cruiser.

Na hii ni maana yake Ahadi ya Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Anderson Lukelo Willilo kurejea nchini na Medali nyingi inaelekea kabisa kutimia.

“Vijana walijiandaa vizuri, kazi iliyokuwa imebakia tulimkabidhi Mungu tu, Mweza wa yote, hakika tunamshukuru kwa hatua tuliyofikia mpaka sasa pamoja na Dua za Watanzania wote waliotuombea mema,” alisema Willilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live