Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changalawe ashinda medali Mandela Cup

Changalawe Ashinda Medali Mandela Cup Changalawe ashinda medali Mandela Cup

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa kikosi cha taifa cha Ngumi cha Faru Weusi wa Ngorongoro Yusuf Changarawe ameshinda medali ya fedha licha ya kupoteza pambano lake la fainali dhidi ya Pita Kabeji kutokea DR Congo kwa pointi 4-3 katika mashindano ya Mandela Cup ndani ya Jiji la Durban, Afrika ya Kusini.

Pambano hilo la uzani wa Light Heavyweight kilo 80 ni la pili kuwakutanisha Changarawe na Kabeji huku Changarawe akipoteza kwa mara ya pili dhidi ya Kabeji baada ya pambano la awali la nusu fainali katika mashindano ya Afrika Accra 2023 lililofanyika mwezi uliopita.

Changalawe amepata medali ya Fedha na zawadi ya pesa Dola $3,000 (sawa na Sh milioni 7.8

Wakati huohuo, Bondia Azizi Chala aliyeshika nafasi ya tatu baada ya kupoteza pambano lake la nusu fainali dhidi ya Trofimus Johannes kwa pointi 5-0 amepata medali ya Shaba na zawadi ya pesa ya Dola $1,500 sawa za Sh milioni 3.8.

Tanzania iliwakilishwa na wachezaji 5 ambao ni Ezra Mwanjwango, Musa Maregesi, Yusuf Changalawe, Aziz. Mashindano hayo yakifikia tamati usiku wa Jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live