Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwanga, Mkola wamuibua Ibrah Class

WhatsApp Image 2024 05 15 At 10.53.29.jpeg Bwanga, Mkola wamuibua Ibrah Class

Wed, 15 May 2024 Chanzo: dar24

Bondia wa ngumi za kulipwa, Ibrahim Mgender ‘lbrah Class’ amesema pambano la Said Bwanga na Said Mkola litakuwa kali kutokana ubora wa mabondia wote wawili.

Bwanga na Mkola watacheza pambano la ‘Dar Boxing Derby’ la utangulizi la raundi nane, uzito wa kati litakalofanyika Juni 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini humo lbrahimn Class amesema, pamoja na wawili hao kufanya mazoezi, lakini Mkola atapigwa kutokana na ubora wa mpinzani wake.

“Mkola ana maneno mengi kuliko kupigana, hivyo awamu hii amekutana na bondia asiyekuwa na maneno.

“Najua uwezo wa Mkola atapigwa raundi za mapema kabisa, kwa sababu Said Bwanga na Mkola ni tofauti sana, Bwanga ana uwezo mkubwa,” amesema ibrahim Class.

Ibrahim Class ameeleza kuwa siku hiyo Mkola anaenda kukatwa kauli ya kuongea na kufundishwa namna ngumi zinavyochezwa ulingoni.

“Tatizo la Mkola ana maneno mengi kuliko kuonyesha kazi, wakati wake umefikä siku hiyo ataonyeshwa namna ya kucheza ngumi na Bwanga,” alisema lbrahim Class.

Naye, bondia Bwanga amesema hana hofu na uwezo wa mpinzani wake kwa sababu anatambua namna anavyocheza.

“Mashabiki zangu wajitokeze kwa wingi siku nimejipanga kutoa dozi kali, pia hiyo kwani kuonyesha utofauti kati yangu na Mkola,” amesema Bwanga

Chanzo: dar24