Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia wa Malawi azimwa fedha za pambano Bongo

Henock Phiri Azikwa Mkwanja Bondia Hannock Phiri wa Malawi

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Hannock Phiri wa Malawi, amesema Hadi sasa hajapata malipo ya pambano lake la Januari 28, alipocheza dhidi ya Adam Lazaro kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Phiri ambaye alishinda TKO raundi ya 4, amesema alikubaliana na Promota wa pambano hilo Ally Mwazoa angemtumia pesa yake lakini hadi sasa hajafanya hivyo.

Bondia huyo anasema, Kila mara anapomkumbusha kuhusu pesa yake, anamjibu atamtumia atulie.

Alipotafutwa Promota wa pambano hilo, simu yake iliita mara kadhaa bila kupokelewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live