Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia apigwa ngumi, atapika ulingoni

Bondia Pic Data Bondia apigwa ngumi, atapika ulingoni

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hii ni kali ya mwaka, baada ya bondia mmoja huko nchini Marekani kupigwa konde kali na kuanza kutapika ulingoni.

Bondia huyo wa ngumi za kulipwa ambaye hana historia nzuri kwenye ngumi Marquez Greer, aliwaacha hoi mashabiki wa ngumi baada ya kupigwa ngumi kali na Marquis 'Hancho' Williams, akapepesuka na kuanguka chini, lakini wakati akijipanga kuamka alianza kutapika mfululizo.

Greer hana historia nzuri kwenye ngumi kuanzia ameanza kupigana akiwa ameshapanda ulingoni mara 15, akiwa amepigwa mapambano yote, lakini tukio hilo la juzi linaonekana kuwa la kihistoria kwake.

Hili lilikuwa pambano la uzito wa kati 'middleweight' na lilikuwa limeshafika raundi ya nne, ambapo bondia huyo alionekana kuzidiwa kwenye raundi zote za awali kabla hajadondoka chini.

Awali kabla hajapingwa ngumi iliyomdondosha, staa huyo mwenye miaka 26 alipigwa ngumi mbili za kichwani na baadaye kutandikwa ya tumbo iliyompeleka chini moja kwa moja na wakati akijaribu kunyanyuka ndiyo hali hiyo ikamtokea.

Sheria za ngumi zinasema kuwa kama bondia atatapika ulingoni basi mwamuzi atatakiwa kumaliza pambano na kumpa mpinzani wake ushindi wa TKO na ndicho kilichotokea baada ya tukio hilo mwamuzi alimtangaza mpinzani wa Green Willians kuwa mshindi wa pambano hilo.

Chanzo: Mwanaspoti