Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Yusuf Changalawe aangukia pua Thailand

Yusuf Changalawe.jpeg Bondia Yusuf Changalawe aangukia pua Thailand

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Yusuf Changalawe, nahodha wa Timu ya Taifa Tanzania ya Ngumi amepoteza pambano lake la kwanza jana katika mashindano ya mwisho ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 kwa matokeo ya kutenganisha (split decision) ya points 3-2 dhidi ya mpinzani wake Cedrick Belony-Duliepre kutoka Haiti.

Pambano hilo la kukata na shoka lililofanyika katika Uwanja wa ndani wa Huamark, Bangkok - Thailand na kusimamiwa na mwamuzi Jung Sook CHO kutoka Korea Kusini, liliwashawishi majaji 3 dhidi ya 2 kumpatia ushindi Cedrick mkazi wa Montreal, Canada na kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Majaji 2 waliompa ushindi Changalawe ni kutoka Morocco 29:28 na Bulgaria 30:27 dhidi ya Argentina 30:27, Israel 29:28 na Sri Lanka 29:28 waliompa ushindi Cedrick.

Kwa matokeo hayo sasa yamemtoa Changalawe katika mashindano hayo ya kufuzu yanayoendelea nchini Thailand. Sasa amebakiwa na tumaini moja tu katika nafasi 9 za usawa na upendeleo (Universality places)

Katika safari ya Thailand, Changalawe ameambatana na mwalimu (IBA 1 star) Mohamed Abubakari na mkuu wa msafara na Makamu wa Raisi wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC) Henry Tandau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: