Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Okolie atetea ubingwa wa WBO

Okolieeeeeee Bondia Lawrence Okolie

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Bondia Muingereza Lawrence Okolie ameutetea mkanda wake wa WBO cruiserweight baada ya kumchapa bondia Mpoland Michal Cieslak kwa ushindi wa alama kwa majaji wote watatu (Unanimous decision) mjini london nchini Uingereza kwenye ukumbi wa O2 Arena.

Okolie mwenye umri wa miaka 29, aliyesindikizwa ulingoni na bingwa za zamani wa uzito wa juu duniani Antony Joshua sambamba na bingwa wa uzito wa kati wa UFC Israel Adesanya, alishinda kwa alama kutoka kwa majaji wote watatu kwa alama 117-110, 116-111 na 115-112.

" hili lilikuwa miongoni mwa pambano gumu nililowahi kucheza,mwenzangu alikuwa vizuri kimazoezi na kimbinu,kwangu napaswa kufanya mazoezi zaidi kuwa imara ili pambano lijalo nifanye vizuri zaidi"amesema Okolie ambaye wazazi wake wanaasili ya Nigeria.

Okolie anafikisha mapambano 18 kucheza mpaka sasa huku akishinda yote ilhali mapambano 14 akishinda kwa KO's huku kukiwa na uwezekano mkubwa pambano linalofuatia kupambana na bingwa wa IBF Mairis Briedis au bondia Mkongo Ilunga Makabu kwenye pambano linalofuatia .

Chanzo: eatv.tv