Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Mtanzania atinga Robo Fainali ALL AFRCAN GAMES

B25903a3 8209 464a 810b 31238b851362.jpeg Bondia Mtanzania atinga Robo Fainali ALL AFRCAN GAMES

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Ezra Paulo Mwanjwango amefanikiwa kutinga Robó Fainali ya Michezo ya Afrika (All African Games) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda kwa RSC (Refa Kusimamisha Pambano) William Mohamed wa Shelisheli

Ilikua katika round ya pili, Dk ya 2 na Sekunde 38 ambapo Kamanda huyo wa Kikosi cha Faru Weusi wa Ngorongoro aliweza kuwainua mashabiki wake kwa kumaliza pambano hilo kwa RSC, refa akisitisha pambano kumuokoa na kipigo zaidi mpiganaji wa Shelisheli.

Bondia mwingine wa Tanzania Abdallah Mafaume ‘Nachoka’ ametolewa na Gerald Kabinda wa Zambia kwa pointi 5-0 uzito wa Welter Hatua ya 16 Bora.

Anakuwa bondia wa pili wa Tanzania kutolewa baada ya Abdallah Abdallah ‘Katoto’ aliyelazimika kujiuzulu juzi katika raundi ya mwisho akipigana na Wibshet Bekele wa Ethiopia kufuatia kuvunjika mkono, ingawa alikuwa anaongoza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live