Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Mtanzania amfanya kitu mbaya Bondia kutoka Uzbekistan

Abdul Ubaya Bondia Mtanzania amfanya kitu mbaya Bondia kutoka Uzbekistan

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa Tanzania, Abdul Ubaya, amefanikiwa kunyakua ubingwa wa WBA Asia uzani wa light heavyweight, baada ya kumchapa kwa pointi za majaji wote watatu 'Unanimous Decision' bondia kutoka Uzbekistan Davronbek Kurbonov.

Pambano hilo lililokuwa la raundi 10, limepigwa mchana huu mjini Bangkok nchini Thailand. Ubaya anakuwa bondia wa pili wiki hii kushinda nje ya Tanzania baada ya Pius Mpenda aliyeshinda Dubai.

Kwa ushindi huo, Ubaya anakuwa na rekodi ya kucheza mapambano Saba (7), akishinda matano (5), kupoteza mawili (2), huku mpinzani wake akiwa na rekodi ya kucheza mapambano nane (8), akishinda (6) tena kwa KO na TKO na kupoteza mawili (2).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live