Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Mtanzania aliyebadili uraia asimulia msoto AUSTRALIA

Tarimo+pic Bondia Mtanzania aliyebadili uraia asimulia msoto AUSTRALIA

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By IMANI MAKONGORO BONDIA namba moja nchini, Bruno Tarimo (Vifuaviwili) ameeleza namna alivyopitia msoto nchini Australia, akitafuta nafasi ya kutoka kabla ya hivi karibuni kuchukua hatua ya kubadili uraia.

Bruno anayetambulika kwa sasa kama bondia wa Australia mwenye asili ya Tanzania, alisema tangu 2018 alipokwenda nchini humo kwa mara ya kwanza, nidhamu na uvumilivu ndivyo vilivyomuongoza.

Bingwa huyo wa zamani wa WBA alicheza nchini humo Machi 2018 kwa mara ya kwanza na Bilel Deb na kutwaa taji hilo kabla ya kurudiana naye Agosti mwaka huo na tangu hapo alilowea huko.

“Sikuwa nafahamu lugha nyingine zaidi ya Kiswahili na kichaga, nilipoondoka Tanzania kuja kurudiana na Bilel niliambiwa nitakaa huku kwa miaka minne baada ya pambano,” alisema Tarimo na kusema; alisaini mkataba akiwa Tanzania akiamini ni wa kukaa Australia miaka minne baada ya pambano la marudiano ambalo alipigwa kwa pointi na kuvuliwa ubingwa wa WBA.

“Baada ya pambano niliambiwa nijiandae kurudi Tanzania, nikauliza kuhusu mkataba wa miaka minne ambao nilisainishwa umeishia wapi? Sababu uliandikwa kwa Kiingereza nami, wakati huo sikuwa nafahamu lugha hiyo,” alisema Tarimo na kuongeza; “Niliambiwa mkataba haukukamilika, hivyo nirudi kwanza Tanzania kisha nitajua.”

Alisema hakuona sababu ya kurudi, kwani maisha yake Tanzania yalikuwa magumu, hata aliposhinda taji la WBA ambalo ni miongoni mwa mataji makubwa ya ngumi za kulipwa, hakuna sapoti yoyote aliyopata

Chanzo: mwanaspoti.co.tz