Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Mtanzania achapwa raundi ya kwanza Russia

78742 Bondia+pic

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Dakika tatu za raundi ya kwanza zilitosha kumaliza pambano la bondia uzito wa juu namba moja Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo baada ya kupigwa kwa Technical Knock Out (TKO) nchini Russia.

Katika pambano hilo, makonde mawili ya kulia ya bondia wa Russia, Arslan Yallyev yalitosha kumpeleka chini Mchumitumbo mara mbili na kujikuta akisalimu amri.

Kocha aliyeambatana na bondia huyo, Anthony Rutha alisema refarii alilazimika kumaliza pambano baada ya Mtanzania huyo kupelekwa chini mara mbili mfululizo.

"Refarii alitoa ushindi wa TKO kwa mpinzani wake, japo Mchumiatumbo alianza vizuri dakika ya kwanza ya pambano, lakini dakika mbili za mwisho za raundi ya kwanza alizidiwa kimbinu na mpinzani wake.

Alisema katika dakika hizo, Mtanzania huyo aliangushwa chini mara mbili na mpinzani wake, hivyo refarii akalazimika kumaliza pambano hilo lililokuwa la raundi nane la uzani wa juu.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz