Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Maono Ally amlilia Twaha Kiduku

Screenshot 20230615 083411 Facebook Bondia Maono Ally amlilia Twaha Kiduku

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Maono Ally Daud a.k.a "The Monster Of Bagamoyo" ameingia kwenye trending za mchezo wa Masumbwii kutokana taarifa yake ya kumtaka bondia kinara wa uzito wa Kg 76 bwana Twaha Kassimu Rubaha a.k.a "Twaha Kiduku".

Maono huyu ni bingwa anayemiliki mkanda wa WBC (World Boxing Council Youth Middleweight Kg 72 Title) mkanda aliyoshinda nnje ya nchii Tarehe 23/2/2018 kwa kumpiga bondia Luka Pupek raia wa Croatia.

Kwa sasa Maono ni mmoja kati ya mabondia watatu bora hapa nchini Tanzania ambao ni tishio kwenye mchezo wa Ndondi hii imekuja baada ya kustrago sana kwaku wataka wapinzani wake mbali mbali ambao niwa wakubwa kwenye mchezo huu wa Ndondi lakini wengi wao wamekuwa wakimkimbia kwa kukataa baadhii ya mapambano dhidi yake toka alivyo kuwa akicheza uzito wa kg 69 na kg 72.

Kwa siku nyingi bondia Maono amekuwa akimlilia sana bondia Kiduku bingwa anayemiliki mikanda ya UBO Inter Continental Title, UBO African Title, WBF International Title na PST Tanzania Title kwenye uzito wa Super Middleweight Kg 76 ili apate nafasi ya kucheza naye.

Lakini ombi lake hilo limekuwa gumu kufanikishwa kutokana na mpinzani wake huyo kuchomoa baadhii ya mapambano dhidi yake.

Kupitia clip ya video inayo sambaa mitandaoni bondia Maono alisema na nukuu "Habari mapromota mimi ni bondia Maono Ally ombi langu kwenu ni kilio changu cha kumtaka bondia na mpinzani wangu Twaha Kiduku ndani ya ulingo.

Kama yeye Kiduku aliomba nafasi ya kucheza na bondia Dullah Mbabe akapewa na mimi na waomba Mapromota nisikilizwe ombi langu la kumtaka bondia Kiduku nimepanda Kg kwa sasa nacheza uzito wa Super Middleweight Kg 76 kg 69 na kg 72 huko kote nishamaliza kuwapiga.

Naombeni mapromota mnifanikishie ombi langu hata Kiduku akikataaa basi nipo ladhii kucheza na bondia yoyote bora kwenye uzito wa Kg 76 ambaye ni mkubwa nipo radhii kucheza naye naomba mapromota hitaji langu lisikilizwe" mwisho wa kunukuu.

Maono ana jumla ya Mapambano 21, Kashinda 13, Kwa "KO'S" 9, Kapoteza 7 na sare 1.

Kiduku ana jumla ya Mapambano 31, Kashinda 22, Kwa "KO'S" 8, Kapoteza 8 na sare 1.

Hizo ndo rekodi za mabondia hao wote wawili kuelekea kwenye pendekezo hilo la bondia Maono la kumtaka bondia Kiduku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live