Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Majiha amtamani Tonny Rashid

Dresss 357.png Bondia Majiha amtamani Tonny Rashid.

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Fadhill Majiha amesema yupo tayari kupanda ulingoni kuzichapa na Tony Rashidi, endapo atatokea promota wa kuandaa pambano hilo.

Majiha mwenye umri wa miaka 29, anashikilia nafasi ya pili katika uzani wa Super Bantam wakati Rashid anashikila nafasi ya kwanza katika uzani huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Majiha amesema kama itatokea ofa yupo tayari kuzichapa na Rashidi kwa kuwa ni bondia mzuni mwenye kuufahamu mchezo huo.

“Rashidi ni bondia mzuri anatambua anafanya nini akiwa ulingoni, kama itatokea ofa hiyo nipo tayari kucheza naye.” amesema Majina.

Kocha wa Rashid Amos Nkondo ‘Amoma’, amesema pia bondia wake yupo tayari kupanda ulingoni na Majiha kama atapewa ofa nono.

“Tupo tayari kucheza kwa sababu hii ni kazi ambayo inatuweka mjini,” amesema Amoma.

Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Saada Kasonso, amesema kuwa, yupo tayari kuandaa pambano la mabondia hao ili kumaliza tambo zinazoendelea mitaani.

“Nipo tayari kuandaa pambano kati ya Majiha na Rashidi kwa sababu wanafanya vizuri,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live