Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Kidunda kusaini kimya kimya

Selemani Kidunda Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Seleman Kidunda

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Imefahamika kuwa Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Seleman Kidunda kesho Jumanne (Januari 16) anatarajia kusaini mkataba wa pambano la kimataifa la kuwania mkanda wa WBF Intercontinental dhidi ya Asemahle Wellem wa Afrika Kusini.

Kidunda anatajwa kupanda ulingoni na bondia huyo kutoka Afrika Kusini ambaye aliwahi kumtandika Twaha Kiduku kwa pointi Julai mwaka jana katika pambano la mkanda wa Ubingwa wa WBF Intercontinental.

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa mpaka sasa makubaliano ya mabondia hao yamefikia pazuri na wanatarajia kusaini mkataba kesho Jumanne (Januari 16) tayari kwa pambano hilo ambalo linatajwa kupigwa Februari mwaka huu.

“Ni kweli Kidunda, anatarajia kupanda ulingoni na Asemahle kwa sababu washafikia makubaliano, japokuwa inafanywa kuwa siri kubwa lakini ukweli ni kwamba jamaa wameshafikia pazuri na bado zoezi la kusaini ambalo limepangwa kufanyika kesho,” amesema mtoa taarifa.

Hata hivyo alipotafutwa Seleman Kidunda hapatikana katika simu yake ingawa inafahamika kuwa pambano kati ya mabondia hao litapigwa Februari, mwaka huu.

Chanzo: Dar24