Wiki hii kwenye Ukumbi wa Next Door Arena jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao watapigana katika pambano la utangulizi la raundi 10, ambapo siku hiyo bondia Hassan Mwakinyo atazichapa na Muangola Antonio Maiala, kuwania Ubingwa wa Afrika wa (ABU) wa uzito wa super welter katika pambano hilo lililoandaliwa na Kampuni ya The Jackson Group Sports chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Kelvin Twissa.
Jongo alisema amejiandaa vizuri na pambano hilo na kamwe hatamdharau mpinzani wake kufuatia ushindi wake mfululizo dhidi ya bondia Alphonce Mchumiatumbo wa Tanzania na Mmarekani Shawn Miller.
Alisema rekodi za Durodoro zinaonyesha jinsi gani bondia huyo alivyo na uzoefu mkubwa katika ngumi za kulipwa kwa kushinda mapambano 34 na kupoteza manane tu wakati yeye mpaka sasa ameshinda mapambano manane, kupoteza moja na kutoka sare mara mbili.
Jongo alisema pambano hilo litamfungulia njia yake ya kucheza kwenye mikanda ya ubingwa wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC), hivyo lazima ashinde.
“Nipo tayari kwa pambano, najua uwezo wa mpinzani wangu na kamwe sitampa nafasi, natarajia upinzani mkali sana,” alisema Jongo.
Durodoro aliyewasili jana alisema kuwa amekuja kuendeleza rekodi yake ya ushindi kwa kumtwanga Jongo.
“Nimekuja kwa ajili ya ushindi na si kushinda, nimejiandaa vema na najua nini cha kufanya siku ya pambano,” alisema Durodoro.
Mbali ya kuwasili kwa Mnigeria huyo na mabondia wawili wa Bulgaria, Pencho Tsvetkov na mwanadada Joana Nwamerue waliwasili mapema zaidi tayari kwa mapambano hayo.
Tsvetkov atazichapa na Mtanzania Daniel Matefu katika pambano la uzito wa juu wakati Joana atazichapa na Mtanzania Leila Yazidu katika pambano la uzito wa super-light.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jackson Group Sports, Kelvin Twissa, alisema kuwa mabondia wengine Sibusiso Zingange, Antonio Maiala na Chris Thompson, watawasili leo wakati bondia kutoka Congo Brazzavile, Ardi Ndembo, atawasili kesho na kwamba tiketi zinauzwa kwa Sh. 50,000 kwa viti vya kawaida na Sh. 200,000 kwa viti maalum kwa njia ya ontapp na Nilipe. Pambano hilo limedhaminiwa na KCB Bank, Tanzania Tourist Board, DStv, Onomo Hotel, M-Bet na Plus Networks Ltd.