Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bondia Ibrahim Class amchapa Said Chino kwa Pointi

IMG 4166 Ibrahim Class.jpeg Ibrahim Class akimtandika Said Chino

Sat, 27 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Ibrahim Class amemchapa mpinzani wake Said Chino kwa pointi katika pambano la raundi 10 lililopigwa usiku huu.

Katika Pambano hilo Bondia Ibrahim Class alionekana kutawala eneo kubwa la mchezo na mpaka raundi 10 zinakamilika amefanikiwa kuzima ngebe za Said Chino.

Akizungumza kwa majigambo baada ya pambano Ibrahim Class anasema;

"Nilishawaambia tangu mwanzo Said Chino sio bondia bali ni mpiga debe wa stendi ya Mbezi na kilichotokea nafikiri wote mmeona"

Nae Said Chino hakuwa nyuma alijaribu kuutangazia umma kuwa anahitaji mechi ya marudiano baina yao kwani hajaridhika na ushindi wa mpinzani wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live