Bondia wa kike Tanzania, Feriche Mashauri amesema kuwa ikitokea akacheza pambano na akapigwa, mume wake huwa anamsaidia kumkanda majeraha ili arejee katika hali yake ya kawaida.
Bondia huyo maarufu amesema kuwa, licha ya kucheza ngumi za kulipwa lakini akifika nyumbani majukumu yake yote kama mwanamke na mama wa familia huyatimiza ipasavyo bila kujali status yake.
"Nikipigwa mume wangu huwa ananikanda na kuniogesha, nikiumia kwenye pambano ulingoni tukifika nyumbani mume wangu huwa anapasha maji ya moto ananiogesha na ananikanda nilipoumia, ananijali sana.
"Ninapokuwa nyumbani huwa nasimama kama Mke, siruhusu House girl afanye usafi au kazi ambazo zinamuhusu mume wangu, usipokuwa makini dada wa nyumbani anaweza kukuibia mume," amesema Feriche Mashauri.