Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangi yamnyima ushindi Mike Tyson

Tyson Bangi W.jpeg Mike Tyson

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unamkumbuka ANDREW GOLOTA, bondia wa masumbwi ya uzito wa juu, aliyevunjwa mfupa wa shavu na kuteuliwa shingo na MIKE TYSON, mwaka 2000?.

Licha ya Pambano kuwa la raundi 10, lakini raundi mbili tu zilimfanya GOLOTA, ashindwe kuendelea na pambano, kutokana na majeraha alioyapata kufuatia ngumi kali za moto za TYSON.

Baadae baada ya kupelekwa hospitali, aligundulika kuwa alipata mvunjiko wa mfupa wa shavu unaounganisha pua, kupita chini ya jicho na kuteuka shingo.

Mwamuzi wa pambano hilo FRANK GARZA, alimpa ushindi wa 'Technical Knock out' (TKO), MIKE TYSON, ushindi ambao bodi ya kusimamia michezo ya Michigan, iliubadili na kuufanya 'No Contest' (Hakuna mshindi).

Hiyo ni baada ya vipimo kuonesha MIKE TYSON alitumia bangi kabla ya kupanda ulingoni kuzichapa na GOLOTA. Ambapo alikataa kutoa vipimo vya mkojo kabla ya pambano. Kwa kosa hilo baadae bodi hiyo ilimfungia MIKE TYSON miezi mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live