Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BFT warudisha salamu za shukurani serikalini

BFT BFT BFT warudisha salamu za shukurani serikalini

Sat, 9 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT) umeishukuru serikali kwa kuiwezesha timu yao ya ndondi kushiriki mashindano ya kufuzu kwa Olimpiki Kanda ya Afrika Dakar, Senegal.

Timu hiyo iliondoka jana Ijumaa (Septemba 08) majira ya alfajiri na mabondia sita, wanne wakiwa wa kiume na wawili wa kike.

Michezo ya Olimpiki itafanyika Paris, Ufaransa mwakani.

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga amesema kuwa anaishukuru serikali kufanikisha safari hiyo baada ya kutoa tiketi za ndege pamoja na posho za wote waliomo katika msafara huo.

Makore amewataja mabondia hao kuwa ni Yusuph Changarawe (kilo 80), Musa Malegesi (kilo 92), Mwalami Salum (kilo 57) na Abdallah Mohamed (kilo 51) wakati wanawake ni Zulfa Macho (kilo 50) na Grace Mwakamele (kilo 60).

Mkuu wa msafara ni Rais wa BFT, Lukelo Wilillo, Viongozi wengine ni Mashaga (kocha msaidizi), Samuel Kapunga (Kocha Mkuu) na Aisha George (matroni).

Mashaga amesema ni matumaini yake kuwa mabondia hao wamejiandaa vizuri na ana matumaini watafuzu kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Haya ni mashindano ya pili ya ndondi ya kufuzu kwa Olimpiki baada ya yale ya Ulaya yaliyotoa mabondia 44, na mengine yatafanyika Busto Arzizi, Italia kuanzia Februari 29 hadi Machi 12, 2024 wakati mengine yatafanyika Bankok, Thailand Mei 23 hadi Juni 3, 2024.

Hivi karibuni mabondia Changarawe na Grace walishiriki mashindano ya ndondi ya Afrika Yaounde, Cameroon na kuvuna mamilioni ya fedha baada ya kutwaa medali za shaba na fedha.

Chanzo: Dar24