Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BFT kutangaza timu ya Taifa

BFT BFT kutangaza timu ya Taifa

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) linatarajiwa kutangaza Timu ya Taifa itakayoingia kambini kujiandaa na mashindano ya All African Game yatakayofanyika Machi mwakani nchini Ghana.

Majina hayo yanatangazwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya bingwa wa mabingwa yaliyofanyika mkoani Iringa mwishoni mwa juma lililopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kupitia mashindano ya Iringa wapo waliofanya vizuri ambao wataingia katika timu ya taifa.

“Tunahitaji kujiandaa na mashindano ya All African Game yatafanyika Ghana sambamba na mashindano ya kufuzu Olimpiki tayakayofanyika nchini Italia mwezi Februari, kwa hiyo tayari tuna majina ya waliofanya vizuri tutatangaza juma hili,”amesema.

Amesema kwa jinsi alivyoona mabondia waliopo wana uwezo wa kwenda kushindana na kufanya vizuri kimataifa na kwamba wanahitaji kuwa kambini mapema kujimaarisha.

Miongoni mwa mabondia waliofanya vizuri hasa katika mashindano ya bingwa wa mabingwa ni Abdallah Maganga, Idd Athuman, Mzonge Hassan, Aziz Chala, Stephano Mika, Hassan Mrutu, Abdallah Mfaume, Joseph Philipo, Eliankunda Daniel, Juma Thabiti, Mussa Wambura, Aisha Idd na Rachel Peter.

Chanzo: Dar24