Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anthony Joshua kutetea ubingwa katika uwanja wa Tottenham Hotspur

97687 Pic+joshua Anthony Joshua kutetea ubingwa katika uwanja wa Tottenham Hotspur

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, Uingereza , Anthony Joshua leo amethibitisha kuwa atatetea mkanda wake wa ngumi za uzito wa juu kwa kupambana na Kubrat Pulev jijini London Juni 20.

Bondia huyo Muingereza alituma katika akaunti yake ya Twitter picha yake akiwa amevalia mkanda huo na kuandika chini yake "Juni 20"

Joshua alifanikiwa kurudisha ubingwa wake unaotambuliwa na vyama vya WBA, IBF na WBO kwa kushinda kwa pointi katika pambano lake dhidi ya Andy Ruiz Jr nchini Saudi Arabia mwezi Desemba.

Ushindi huo ulimuwezesha Mwingereza huyo kulipa kisasi cha kushindwa kwa mara ya kwanza tangu aanze ngumi za kulipwa baada ya kupigwa na Ruiz mwezi Juni mwaka jana jijini New York.

Joshua atapambana na Pulev, ambaye ni raia wa Bulgaria katika pambano litakalofanyika kwenye uwanja mpya wa klabu ya Tottenham Hotspur kaskazini mwa London.

Pulev, ambaye ndiye anayetakiwa kikanuni kuwania mkanda wa IBF unaoshikiliwa na Joshua, alijiondoa katika pambano dhidi ya Mwingereza huyo ambalo lilikuwa lifanyike mwaka 2017 kutokana na kuumia.

Pia Soma

Advertisement
Pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu baina ya mabondia wa Uingereza, Joshua na Tyson Fury liliingia dosari wakati Mmarekani Deontay Wilder aliposema atalazimika kutumia kifungu katika mkataba wake cha kupambana kwa mara ya tatu na bingwa mpya anayetambuliwa na WBC.

Chanzo: mwananchi.co.tz