Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amir Khan atamba kumchapa Kell Brook

BOXING 2022 Kell Brooks (kushoto) na Amir Khan

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Bondia Amir Khan ametamba kumpiga Kell Brooks kwenye pambano maalum la kumaliza ubishi kati ya wapizani hao wa muda mrefu la SuperWelter Weight (Uzito wa kati) linalotaraji kuchezwa Jumamosi ya Februari 17, 2022 kwenye Ulingo uliopo Manchester nchini England.

Bondia Amir Khan ametamba kumpiga Kell Brooks kwenye pambano maalum la kumaliza ubishi kati ya wapizani hao wa muda mrefu la SuperWelter Weight (Uzito wa kati) linalotaraji kuchezwa Jumamosi ya Februari 17, 2022 kwenye Ulingo uliopo Manchester nchini England.

Khan (35) amesema “Itakuwa kitu cha kunisikitisha sana kwenye maisha yangu ya ngumi kama nikipoteza kwa Kell Brook. Hiyo ndiyo sababu ya kwenda kwenye mpambano huo nikiwa tayari kwa 100% na natakiwa kumpiga kwa namna nzuri”.

“Kila mtu anaona hatupendani. Siwezi kupoteza kwa mtu kama Kell Brook” aloingeza Amiri Khan.

Naye Brooks (35) amejigamba kumshushia makonde na kumshinda Amir Khan kwa kupunguza uzito wake katika pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu na wafuasi wengi wa ndondi England na Ulimwenguni kiujumla.

Mara ya mwisho Khan kushuka ulingoni ilikuwa miaka mitatu iliyopita (2019) wakati Brooks alishuka dimbani Novemba 2020 tena akiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mapambano matatu kati ya sita aliyoshuka Ulingoni.

Amir Khan amecheza mapambano 39, ameshinda mara 34, 21 akishinda kwa Knock-Out (KO) na kudundwa mapambabo 5. Kell Brook amecheza mapambano 42, ameshinda 39, 27 kwa Knock-Out (KO) na kupigwa mara 3.

Pambano hilo litafanyika Manchester Arena yenye uwzo wa kubeba watazamaji 21,00 nchini England na tokea kutangazwa kwake wafuasi na wapenzi wa mchezo huo wameshanunua ticket zote ndani ya dakika 10.

Chanzo: eatv.tv