Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amir Khan Apewa Wiki Tatu

Amir Khan Amir Khan Apewa Wiki Tatu

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

OFISA Mtendaji Mkuu wa taasisi ya ngumi ya Boxxer, Ben Shalom, amesema Muingereza Amir Khan ana wiki tatu tu za kuhuisha kipengele cha kuomba mechi nyingine dhidi ya mpinzani wake Kell Brook, la sivyo, hawawezi kucheza tena.

Khan alikumbana na kichapo cha TKO katika raundi ya sita dhidi ya Brook wiki iliyopita katika pambalo lisilo na ubingwa lililochezwa kwenye Ukumbi wa Manchester.

Shalom alisema: “Watu hawajui kama Amir Khan ana kipengele cha kuomba mechi nyingine katika mkataba. Lakini siyo kitu tunachomshauri na ni kitu ambacho hatudhani kama atafanya, lakini ana kipengele hicho. Nilichokiona ilikuwa ni vita ya mtu mmoja na nadhani Amir alimalizwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live