Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikuwa na maneno ya kutupa moyo- Mwakinyo 

995f397fe8bd79026ac9b47874f3537e.png Alikuwa na maneno ya kutupa moyo- Mwakinyo 

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Hassan Mwakinyo amesema anamkumbuka Rais wa awamu ya tano John Magufuli alivyowapa moyo wanamichezo kwa kutokubali kushindwa kiurahisi.

Mwakinyo ni miongoni mwa wanamichezo waliopewa viwanja vya kujenga mkoani Dodoma baada ya kufanya vizuri katika pambano lake dhidi ya bondia kutoka Argentina Sergio Gonzalez.

Akizungumza na gazeti hili jana Mwakinyo alisema anakumbuka siku waliyokwenda kula naye chakula Ikulu aliwauliza kwanini wanakubali kushindwa na watu ambao wanafanana.

“Nakumbuka alisema kwanini tunashindwa? Maneno yake yamekaa moyoni mwangu ndio maana huwa sikubali kushindwa katika mapambano, kwasababu kila nikikumbuka napata ujasiri wa kupambana,”alisema.

Alisema kwa mawazo yake ili kumuezi Rais huyo aliyefariki dunia Jumatano ya wiki hii, itapendeza mabondia wenzake wakawa na fulana maalum zenye maneno yake ya ushindi.

Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa hizo fulana ziwe zinavaliwa kipindi ambacho wanapata mapambano ya nje wawe wanavaa kutangaza mazuri ya kiongozi huyo.

Bondia huyo alisema ikiwa watashirikiana na wengine kufanya hivyo, maneno yake ya ushindi na ujasiri yatazidi kuishi mioyoni mwao.

Mwakinyo alikuwa na pambano hivi karibuni limesogezwa mbele kupisha maombolezo ya kifo cha Magufuli anayetarajiwa kuzikwa Machi 25, mwaka huu nyumbani kwao Chato.

Chanzo: www.habarileo.co.tz