Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AJ vs USYK rasmi 2022

Aj Pic Data Bondia Anthony Joshua ‘AJ’

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Amechomoa! Ndivyo ilivyo Bondia Anthony Joshua ‘AJ’ sasa ni rasmi ameamua kutomuachia Mwingereza mwenzake Tyson Fury kupigana na Oleksandr Usyk kwenye pambano lililovuma karibuni, huku kukutana kwao kukiongeza uwezekano huo.

AJ ndiye ameamua iwe hivyo, kwamba anataka kulipiza kisasi cha kupoteza pambano la kwanza lililofanyika Septemba mwaka huu, pale London Uingereza akipigwa kwa pointi za majaji wote watatu na sasa atalipiza kisasi kama alivyofanya kwa Andy Ruiz Jr.

Katika kuhakikisha hilo linatimia, AJ pia ameamua kuhama kambi yake ya mazoezi iliyopo Sheffield nchini kwao Uingereza akitarajiwa kuweka kambi nchi nyingine ambayo bado haijawekwa wazi, ikiwa na kocha mpya.

Hii inamaanisha kwamba, kwa muda mfupi hatakuwa na kocha wake Rob McCracken, bali kuna uwezekano mkubwa AJ akanolewa na kocha wa mabondia wakali kuanzia kwa aliyekuwa anamnoa Floyd Mayweather Jr, Saul ‘Canelo’ Alvarez au kocha wa ndugu yake wa nchi moja, Tyson Fury.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz