Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

16 kumsindikiza Kidunda, Mfaume

Image 275.png 16 kumsindikiza Kidunda, Mfaume

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Mabondia 16 wanatarajia kupanda ulingoni katika mapambano nane ya utangulizi kuelekea pambano la Seleman Kidunda dhidi ya Eric Mukadi.

Pambano hilo, linatarajiwa kupigwa Juni 30, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mbali ya Kidunda ambaye atacheza na Mukadi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Bondia Mfaume Mfaume atapanda ulingoni katika pambano hilo dhidi ya Mkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini katika pambano hilo kabla ya Kidunda kuzichapa.

Promota wa pambano hilo, Fadhili Maogola alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri ambapo jumla ya mapambano 10 yatakawakutanisha mabondia 20 wakiwemo watatu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

“Kwanza tunamshukuru Mungu, Maandalizi pambano letu ya yanakwenda vizuri, mapambano yote yatakuwa 10 yakiwa na jumla ya mabondia 20, nane yatakuwa ya utangulizi na kisha Kidunda kufunga dimba na Mukadi,” amesema Maogola.

Promota huyo alitaja mapambano ya utangulizi ambayo ni Fadhili Majiha Stopper atapanda ulingoni dhidi ya Jamal Kunoga wakati Saleh Kasim atamalizana na Said Bwanga kabla ya Deo Samweli kumvaa Adam Ngange.

Wengine ni Pius Mpenda ambaye atapanda ulingoni dhidi ya Simon Tichecha wa Malawi wakati Rama John akitarajia kupasuana na Yonas Segu huku Omary Maulid atapanda na Shaban Kibiriti huku Boniface Seguda atacheza na Hamza Mahamoudu naye Herry Rashid akitarajia kumalizana na Hussein Pendeza.

Chanzo: Dar24