BBC

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuAfrika
BBC

Wagonjwa wa saratani ya ngozi ya melanoma waongezeka Uingereza

Wagonjwa Wa Saratani Ya Ngozi Ya Melanoma Waongezeka Uingereza Wagonjwa wa saratani ya ngozi ya melanoma waongezeka Uingereza

Mon, 27 May 2024 Chanzo: BBC

Shirika la misaada la saratani linawaonya watu kuchukua hatua zaidi kujikinga na jua huku idadi ya wagonjwa wa saratani ya ngozi ya melanoma nchini Uingereza ikiendelea kuongezeka.

Utafiti wa Saratani Uingereza unatabiri kutakuwa na rekodi ya kesi 20,800 zilizogunduliwa mwaka huu, kutoka wastani wa kila mwaka wa 19,300 kati ya 2020 na 2022.

Uchambuzi wake unaonesha viwango vilivyoongezeka kwa karibu theluthi kati ya 2009 na 2019, kutoka kesi 21 hadi 28 kwa kila watu 100,000.

Kuongezeka kwa utambuzi kunatokana na kuongezeka kwa watu wazee na kuongezeka kwa ufahamu wa ishara za saratani ya ngozi.

Ripoti hiyo inaeleza takribani visa 17,000 vya melanoma kila mwaka vinaweza kuzuilika na karibu tisa kati ya 10 husababishwa na mionzi mingi ya ultraviolet (UV).

Melanoma ni aina mbaya ya saratani ya ngozi ambayo inaweza kuenea kwa sehemu nyingine za mwili. Pia kuna saratani za ngozi zisizo za melanoma, ambazo kwa ujumla ni za kawaida zaidi na kawaida sio mbaya kuliko melanoma.

Kulingana na Utafiti wa Saratani (CRUK) kuongezeka kwa kesi kumefunika makundi yote ya umri lakini ongezeko kubwa zaidi ni katika makundi ya wazee, hasa kwa watu wazima zaidi ya miaka 80, ambapo uchunguzi umeongezeka kutoka kesi 61 hadi 96 kwa kila watu 100,000 kwa muongo mmoja.

Pia kumekuwa na ongezeko kati ya watu wazima wenye umri wa kati ya miaka 25 na 49, kulingana na uchambuzi.

Kwa kundi hili kiwango kimepanda kutoka 14 hadi 15 kwa watu 100,000 kwa miaka 10. Vijana wana uwezekano mkubwa wa kufahamu uhusiano kati ya UV na saratani ya ngozi kuliko vizazi vya zamani, wanasayansi wanaeleza. Hii inaweza kumaanisha kuwa wana uwezekano mkubwa wa kuchukua tahadhari juani, ikilinganishwa na wazee, ambao walikua hawafahamu hatari za kujianika juani.

Chanzo: BBC