BBC

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuAfrika
BBC

Tukio la kwanza duniani la mtu kuambukizwa mafua ya ndege

Maafisa Marekani Wataja Tukio La Kwanza Duniani La Mtu Kuambukizwa Mafua Ya Ndege Maafisa Marekani wataja tukio la kwanza duniani la mtu kuambukizwa mafua ya ndege

Thu, 23 May 2024 Chanzo: BBC

Mfanyakazi mmoja wa shamba la Michigan amegunduliwa ana ugonjwa wa mafua ya ndege ikiwa ni kisa cha pili cha binadamu kuhusishwa na mlipuko katika eneo lenye ng'ombe wa maziwa Marekani.

Maafisa wa afya wanasema mtu huyo alipata dalili za ugonjwa wa macho kidogo na amepona. Maafisa wanasema mfanyakazi huyo alikuwa karibu na ng'ombe kwenye shamba lililokuwa na mifugo iliyoambukizwa.

Maafisa wanasema hatari kwa umma bado ni ndogo, lakini wafanyakazi wa shamba walio karibu na wanyama walioambukizwa wako katika hatari kubwa zaidi.

Mfanyakazi mmoja wa shamba la Texas aligunduliwa mwishoni mwa Machi katika hali kama hiyo. Maafisa walitaja tukio hilo la kwanza kujulikana duniani kote la mtu kuambukizwa aina hii ya mafua ya ndege kutoka kwa mnyama.

Chanzo: BBC