BBC

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuAfrika
BBC

Sunak atangaza uchaguzi mkuu wa Uingereza utafanyika Julai 4

Sunak Atangaza Uchaguzi Mkuu Wa Uingereza Utafanyika Tarehe 4 Julai Sunak atangaza uchaguzi mkuu wa Uingereza utafanyika tarehe 4 Julai

Thu, 23 May 2024 Chanzo: BBC

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameapa "kupigania kila kura" alipokuwa akiitisha uchaguzi mkuu wa mapema wa Uingereza Alhamisi tarehe 4 Julai.

Waziri Mkuu alitoa tangazo hilo katika hotuba yake, wakati akijipigia debe kushinda muhula wa tano kwa wahafidhina.

Hatua hiyo ambayo haikutarajiwa ilibadilisha matarajio ya kura, ambayo inaweza kuwa imewapa wabunge wa chama chaConservative fursa nzuri ya kuziba pengo na chama cha Labour.

Sir Keir Starmer alisema ni "wakati wa mabadiliko" kuondokana na "Machafuko ya chama tawala".

Chama cha Labour kimekuwa kikionyesha kuongoza katika kura za maoni za kitaifa, na kimesisitiza kuwa ina kampeni iliyoandaliwa kikamilifu na tayari kuanza.

Bunge sasa litasitishwa siku ya Ijumaa, kabla ya kufungwa rasmi Alhamisi wiki ijayo kwa kampeni rasmi ya uchaguzi ya wiki tano.

Ina maana kuna siku mbili tu za kupitisha sheria yoyote ambayo imesalia - hatua ambayo itamaanisha kuwa baadhi ya hatua zilizokusudiwa za serikali zitalazimika kuachwa.

Chanzo: BBC