Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Worrios yainyuka Grizzlies 101-98, wanaongoza 3-1

Gsw.jpeg Stephen Curry amefunga alama 32, ametoa Assist 8 na Rebound 5

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Stephen Curry ameiongoza Golden State Worriors kuibuka na ushindi wa alama 101 kwa 98 dhidi ya Memphis Grizzlies. Kwenye mchezo wa nusu fainali ya 4 kwenye mfululizo wa michezo 7 ya nusu fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA hatua ya mtoano (Play Off) ukanda wa Magharibi.

Ushindi huu unaifanya Golden State kuongoza kwa ushindi wa michezo 3-1 kwenye michezo 4 ya nusu fainali waliocheza. Katika mchezo huu Stephen Curry amefunga alama 32, ametoa pasi za kufunga (Assist) 8 na Rebound 5.

Mchezo mwingine wa nusu fainali uliochezwa leo Alfajiri ukanda wa Mashariki Boston Celtics wameinyuka Milwaukee Bucks kwa ushindi wa alama 116 kwa 108. Na kufanya timu hizi zote kuwa zimeshinda michezo 2 kila timu katika michezo 4 waliocheza.

Kwenye mchezo huu mchezaji nyota wa Celtics Al Horford amefunga alama 30 (Assists) 3 na rebound 8. Jayson Tatum amefunga alama 30, pasi za kufunga (Assists) 5 na rebound 13. Na mchezaji nyota wa Bucks Giannis Antetokounmpo amefunga alama 34 ametoa pasi za kufunga (Assists) 5 na Rebound 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live