Viatu vya aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya kikapu nchini Marekani Chicago Bulls, Michael Jordan,vimeuzwa kwa bei ya dola milion1.47 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 3.45 iliovunja rekodi katika mnada.
Bei hiyo ndio ya juu zaidi kwa viatu vya michezo kuwahi kuuzwa ama kununuliwa duniani.
Jordan alitumia viatu hivyo aina ya Nike Air Ships, vyenye rangi nyekundu na nyeupe wakati wa msimu wake wa kwanza akiichezea timu ya Chicago Bulls, mwaka 1984.
Alipojiunga na Bulls, Jordan na Kampuni ya Nike walianza ushirikiano wa kutengeneza nguo na viatu vyenye nembo yake.
Jordan anaaminika na wengi kuwa mchezaji bora zaidi katika historia ya mchezo wa vikapu.
Jordan ambaye kipindi kirefu aliichezea timu ya Chicago Bulls alikuwa nyota na kuweza kuinua kiwango cha mchezo huo kote duniani.
Jordan ambaye alistaafu mwaka 2003 alikuwa mchezaji wa kwanza bilionea katika historia ya mchezo wa mpira wa kikapu duniani.