Wababe wa NBA Msimu huu Phoenix Suns hatimae wamepata kipigo kingine baada ya zaidi ya mechi 10 za ushindi mfululizo.
Atlanta Hawks ndio nao wamefanikiwa kutibua rekodi ya wakali hao baada ya kuwafunga kwa points 124 - 115.
Mchezaji mahiri Trae Young kama kawaida alikua machachari katika ushindi huo na kufunga points 43 na kuipa Suns kipigo cha 10 baada ya mechi 51 ushindi ukiwa 41.
Hawks wameshinda mchezo wa 25 na wamepoteza 26 mpaka sasa.
Kule LA kulikua na vita ya mahasimu wawili LA clippers na LA lakers ambapo Clippers wakawazima ndugu zao kwa points 111 - 110.
Reggie Jackson amefunga points 25 katika ushindi huo unaowaacha Lakers katika hali mbaya wakiwa wamepoteza mechi 28 na kushinda 25.
Klay Thompson anazidi kuimarika tangu atoke kwenye maumivu na akaiongoza Warriors leo kuipiga Sacramento Kings kwa points 126 - 114.
Klay amepiga pints 23 leo na kutoa asisst 7 huku akipiga mitupo ya points 3 mara 7 katika ushindi huo
Warriors sasa wameshinda michezo 40 na kupoteza 13 na bado ni wapili kwa ubora nyuma ya Phoenix Suns ,wamekua timu ya pili kufikisha ushindi wa mechi 40 msimu huu
Matokeo mengine kama yanavyooneka katika jedwalihapa chini;