Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Stephen Curry mbioni kumpita Allen NBA

STEPH  CURRY 21 Stephen Curry kwenye matukio ya kufunga 3-pointers

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa Golden State Warriors, Stephen Curry yuko mbioni kumpita Hall of Famer, Ray Allen amabye ni kinara wa muda wote kwenye historia ya NBA kwenye orodha ya wachezaji wenye 3-Pointers nyingi zaidi.

Curry alifunga alama 18 kupitia 3-Pointers dhidi ya Portland Trail Blazers siku ya Jumatano na kuongeza pointi 2,964 za pointi 3, jambo ambalo linamfanya abakize pointi 10 tu za 3-Pointers ili kumpita Allen kwenye nafasi ya kwanza.

Mchezaji huyo amefunga walau 3-Pointers moja katika michezo 148 mfululizo, ambayo inaorodheshwa kama rekodi ndefu zaidi ya NBA ya kucheza, na safu ya pili ndefu zaidi katika historia ya ligi baada ya kumpita Kyle Korver (127).

Bingwa huyo mara tatu wa NBA tayari anamiliki rekodi ya muda wote ya NBA ya michezo 157 mfululizo akiwa na angalau pointi 3.

Kwa kasi ya sasa ya Curry (ana wastani wa kufunga 3-Pointers 5 katika kila mechi), anaonekana kuwa hadi kufikia Desemba 11-14 tayari atakuwa ameshampita Allen atakapokuwa anacheza dhidi ya  Philadelphia 76ers, Indiana Pacers na New York Knicks.

Mpaka sasa Curry anaongoza katika mbio za Kia MVP wiki hii, alifunga pointi 105 kwa 3-Pointers katika michezo yake 19 tu ya kwanza msimu huu na kuvunja rekodi yake ya NBA (mechi 20) kwa mechi chache zaidi kufikisha pointi 100 kwa 3-Pointer kwa msimu.

Curry na Allen walitajwa kwenye Timu ya Maadhimisho ya Miaka 75 ya NBA.

Chanzo: eatv.tv