Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Staa NBA aliyegomea chanjo asababisha maandamano

Kyrieirving 3 Maandamano ya kushinikiza Kyrie Irving aruhusiwe kucheza NBA

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Maandamano makubwa yamezuka kumsapoti staa wa NBA  Kyrie Irving, anayekiwasha katika timu ya Brooklyn Nets  aliyegomea chanjo ya Corona na kukatazwa kucheza kikapu mpaka akubali kupata chanjo hiyo.

Mashabiki wamejazana katika uwanja wa Brooklyn Nets unaoitwa NYC’s Barclays Center kushinikiza staa huyo aruhusiwe kucheza tena kikapu kwani maamuzi ya kuchanjwa ama kutochanjwa ni ya mtu binafsi.

Video zinazosambaa mitandaoni zinawaonesha mashabiki hao wakiwa kwenye maandamano hayo yaliyoanza tangu jumamosi, zimezua taharuki nchini humo.

Uongozi wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets ulishatoa taarifa mapema mwezi huu kuwa Irving hatoweza kushiriki mashindano ya kikapu mpaka pale atakapokubali kuchoma chanjo ya Corona.

Marekani imewekwa sheria ya kila mchezaji kupata chanjo ya Corona hata kama mchezaji haishi katika taifa hilo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz