Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Rekodi ya Utah Jazz yafikia kikomo NBA

TK Rekodi ya Utah Jazz yafikia kikomo NBA

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Chicago Bulls ilifanikiwa kupata ushindi wake wa tano kati ya michezo sita ya Ligi ya Kikapu nchini Marekani walipoipa kipigo cha kwanza Utah Jazz msimu huu.

Utah Jazz walipokuwa wakionyeshana umwamba dhidi ya Chicago Bulls kwenye mchezo wa NBA

DeMar DeRozan alikuwa kinara kwa kufunga katika mchezo huo akimaliza kwa alama 32 na kuisaidia Bulls kushinda kwa alama 107-99.

Utah Jazz ndio timu pekee iliyokuwa imesalia kucheza bila kufungwa, lakini kipigo cha leo kimefuta mwanzo huo mzuri waliokuwa nao .

Mabingwa watetezi, Milwaukee Bucks wamefungwa 102-93 dhidi ya San Antonio Spurs ambao huo ndio uliokuwa ushindi wao wa kwanza wa ugenini msimu huu.

Washingtong Wizard iliendeleza kasi yake nzuri walipoinyuka Boston Celtics kwa alama 115-112 wakati Ditroit Piston walainyuka Orlando Magic 110-103.

Matokeo mengine Denver Nuggets wakaichapa Minnesota Timberwolves 93-91, Miami Heat iliinyuka Memphis Grizzlies kwa alama 129-103 ambapo Jimmy Butler akifunga alama 27.

RJ Barrett alifunga alama 35 wakati New York Knicks ikiitandika Pelicans kwa alama 123-117, Phidalelphia 76ers ilishinda kwa mara ya pili mfululizo dhidi ya Atlanta Hawks 122-94, nayo Phoenix Suns ikaibuka na ushindi wa alama 101-92 za Cleveland Cavaliers nayo Golden State Warriors ikaibuka na ushindi wa alama 103-82 za Oklahoma City Thunder.

Chanzo: eatv.tv