Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Phoenix Suns waipiga Chicago, Warriors Wakiendeleza moto NBA

Phoenix Suns Vs Chicago Phoenix Suns waipiga Chicago

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Devin Booker amefunga vikapu 38 akiweka mitupo ya points 3 mara 5 katika ushindi wa timu bora msimu huu ukanda wa Magharibi ya Phoenix Suns.

Phoenix Suns wamewafunga Chicago Bulls kwa jumla ya points 127 kwa 124 huku wakiandikisha ushindi wao wa 43 msimu huku wakiruhusu kupoteza michezo 10 pekee.

Golden States taa ya kijani inaendelea kuwawakia kunako @nba mara baada ya leo kuendeleza ushindi wao wa 41 msimu huu kwa kuwafunga Oklahoma City Thunder kwa jumla ya vikapu 110 kwa 98.

Klay Thompson alifunga vikapu 21 na kuiba mipira mara 2 kuwawezesha Warriors kuibuka na ushindi huo.

Pascal Siakam alikua na wakati bora wakati Raptors wakiwatundika Charlotte Hornets kwa jumla ya vikapu 116 kwa 111.

Siakam alifunga vikapu 24, kutoa assists 8, na kudaka rebounds 11 katika ushindi huo wa Raptors.

Matokeo mengine ni kama yanavyoonekana kwenye jedwali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live