Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

OKlahoma yaendelea kuiduwaza LA Lakers

Shai.jpeg Russell Westbrook (Kushoto) akimzuia mchezaji wa Oklahoma City Thunders, Shai Gilgeous-Alexander.

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Oklahoma City Thunders imeendelea kuiduwaza Los Angeles Lakers baada ya Shai Gilgeous-Alexander kufunga pointi 28 huku City Thunder, ikiepuka kipigo cha tofauti ya pointi 19 na kuwalaza Lakers 107-104.

Gilgeous-Alexander, aliongeza rebounds 3 na asisti 6 katika ushindi wa pili pekee wa Oklahoma baada ya mechi nane za msimu huu, ambapo zote wakishinda dhidi ya Lakers.

Kwa upande wa Los Angeles, Russell Westbrook alifunga pointi 27, rebounds 6 na asisti 5 lakini akashindwa kulazimisha muda wa ziada na jaribio la dakika tatu la mwisho kwa Lakers, ambao hawakuwa na LeBron James aliyekosa mchezo kutokana na majeruhi.

Kwingineko, Phoenix Suns waliwashinda Houston Rockets 123-111 na kufikisha ushindi wao wa nne msimu huu.

Ufungaji wa pointi 27 wa Devin Booker ndani ya dakika 34 pekee uliwatia moyo Phoenix kwa usaidizi wa pointi 19 zaidi kutoka kwa Landry Shamet na 16 kutoka kwa Mikal Bridges na Deandre Ayton wakiizamisha Rockets, ambao waliongoza 93-86 katika robo ya tatu, ya mchezo huku Kevin Porter wa kwa upande wa Houston alifunga pointi 20, huku Christian Wood akiongeza 18.

Chanzo: eatv.tv