Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Mtaka awatahadharisha Viongozi TBF

Cf287ea849e2a1affe352095b176e672 Anthony Mtaka

Sat, 1 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Viongozi wapya wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) wametakiwa kufanyia kazi maoni ya wanachama na wagombea ambao hawakuchaguliwa ili kujenga na kuliimarisha shirikisho hilo.

Kauli hiyo ilisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dodoma, Khamis Mkanachi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Dodoma, Anthony Mtaka katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi ambao awali ulitanguliwa na Mkutano Mkuu uliofanyikM hoteli ya Dear Mama jijini Dodoma.

“ Ipo haja mchezo wa kikapu kuendelezwa katika ngazi za wilaya, binafsi nitahakikisha maoni niliyopata hapa nitafanyia kazi ili wilaya ninayoiongoza ya Kondoa kuwa ya mfano” alisema Mkanachi.

Naye Rais mpya wa TBF Michael Kadege aliwahakikishia wanachama wa TBF waliomwamini na kumchagua kwa kura nyingi kuwa atashirikiana na watu wote ili kutimiza malengo yao hususani ya mpira wa kikapu kupiga hatua kubwa kimataifa.

Viongozi wapya wa TBF, Rais ni Michael Kadege aliyepata kura 52 akimshinda Phares Magesa aliyeambulia kura nane, Makamu wa Rais ni Rwehabura Barongo aliyepata kura 44 akiwashinda Mboka Mwambusi aliyeambulia kura tisa na Alphonce Kusekwa aliyepata kura saba.

Nafasi ya Katibu Mkuu ilichukuliwa na Mwenza Kabinda kwa kura 47 dhidi ya mpinzani wake Michael Mwita aliyepata kura 13, Katibu Msaidizi imeenda kwa Benson Nyasebwa aliyepata kura 50 dhidi ya Daniel Kapoma aliyepata kura 10, Mhazini ni Leonard Haule aliyekuwa mgombea pekee aliyepata kura 54 na sita zikimkataa.

Kamisheni ya Walemavu alichaguliwa Azizy Mwaruka kwa kura zote 60 za ndiyo, Kamisheni ya Watoto na Maendeleo ya shule alichaguliwa Ramadhan Bakari kwa kura 29 akimshinda Hamis Mpili aliyepata kura 26, Kamisheni ya Mipango na Maendeleo, Fredrick Mtandu aliibuka mshindi kwa kura 39.

Kamisheni ya Waamuzi mshindi ni Daniel Mbwana kwa kura 38 na Kamaisheni ya makocha Robert Manyerere mgombea pekee aliyeshinda kwa kura 46 za ndiyo huku kura 14 zikimkataa.

Wajumbe 60 ndio waliopiga kura kwenye uchaguzi huo, na safu mpya ya uongozi itaongoza shirikisho hilo kwa miaka minne ijayo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz