Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Mjane wa Kobe Bryant, alipata taarifa za kifo cha mumewe mtandaoni

BeFunky Collage 3 22 Scaled 1 1536x768.jpeg Marehemu Kobe Bryant na mtoto wake (kushoto) , Kulia ni mke wake

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliekuwa mke wa Mcheza kikapu wa marekani Kobe Bryant, ametoa ushuhuda na kudai kuwa alipata taarifa za kifo cha mumewe na binti yao kilichotokana na ajali ya helikopta baada ya kuona ujumbe wa "RIP Kobe" katika simu yake ya mkononi maarufu kama "notification"

Kobe na binti yake Gianna aliekuwa na umri wa miaka 13, na watu wengine saba walipoteza maisha mwezi Januari 2020, pale helikopta waliyopanda kwenda katika mashindano ya Mpira wa Kikapu ilipopata ajali katika milima, mashariki mwa Los Angeles.

Vanessa Bryant alisema aliwaomba watu wa usalama kutoka Los Angeles kuhakikisha hakuna anaeweza kupiga picha kutoka katika eneo ambalo helikopta hiyo ilipata ajali na kuchukua maisha ya nyota huyo wa kikapu.

"Wakati nanapewa taarifa , niliambiwa kwanza kuhusu ajali hiyo, lakini walisema kwamba watu watano walinusurika, alidhani mume wake alikuwa miongoni mwao na kwamba wangekuwa wakitoa msaada kwa wengine".

"Nilikuwa nimeshikilia simu yangu, kwa sababu ni wazi nilikuwa nikijaribu kumpigia tena mume wangu, lakini jumbe ziliingia zikisema: 'RIP Kobe. RIP Kobe. RIP Kobe” Amesema Vanessa

"Maisha yangu hayawezi kuwa sawa bila mume na binti yangu"

Baada ya Sheriff Alex Villanueva kuthibitisha kuwa mumewe na binti yake waliuawa, alimuuliza Bryant kama angeweza kumfanyia chochote.

"Nilimwambia kama huwezi kunirudishia mume wangu na binti yangu, tafadhali hakikisha hakuna mtu anaechukua tukio la kifo chao".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live