Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Matokeo NBA kwa mechi zilizochezwa leo alfajiri

Skysports Clippers Mavericks 5398550 Ligi ya NBA iliendelea Alfajiri ya leo

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Ligi ya kikapu ya nchini Marekani (NBA) imezidi kupamba moto alfajiri ya kuamkia leo takribani michezo kumi ilichezwa.

Trae Young alifunga alama 31, assists 7 na rebounds 5 akiingoza Atlanta Hawks kupata ushindi wa alama102 kwa 99 vya New Orleans Pelicans.

Mapacha wa L.A (Clippers na Lakers) walipoteza. Lakers alichwapwa na Thunder alama 123 kwa 115 huku Clippers akitandikwa na Clevelland Cavaliers kwa alama 92 kwa 79.

Trail Blazers aliinyoa Memphis Grizzles kwa alama116 kwa 96 nayo Brooklyn Nets ikishindwa kufua dafu mbele ya Miami Heat baada yakupasuka kwa alama 106 kwa 96.

Toronto Raptors waliibamiza Indiana Pacers kwa 118 dhidi ya100 nayo Orlando Magic alinyolewa na Charllote Hornets vikapu 120 - 111.

Boston Celtics alipokea kipigo toka kwa Washington Wizards cha alama 99 - 94 nayo Milwaukee Bucks alionja joto la jiwe mbele ya Minnesota Timberwolves baada ya kuchapika kwa alama 113 -108, nayo Sacramento Kings waliichapa Phoenix Suns kwa alama 110 - 107.

Chanzo: eatv.tv