Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

MVP wa NBA afungiwa mchezo mmoja

Jokic.jpeg MVP wa NBA afungiwa mchezo mmoja

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

MVP wa NBA, anayechezea timu ya Denver Nuggets, Mserbia Nikola Jokic, amefungiwa kucheza mchezo mmoja bila malipo kwa kumsukuma kwa nguvu fowadi wa Miami Heat, Markieff Morris wakati wa mechi baina ya pande hizo mbili.

Kusimamishwa kunamaanisha Nuggets hawatakuwa na Mserbia huyo kwenye mechi yao dhidi ya Indiana Pacers siku ya Jumatano alfajiri ya kuamkia Alhamisi.

Morris pia alitozwa faini ya dola za Kimarekani 50,000 (Tshs 115,500,00) kwa makosa yake mawili ya kufanya madhambi yaliyosababisha Jokic kulipiza kisasi, huku Jimmy Butler wa Miami pia ametozwa faini ya dola 30,000 (Tshs. 69,000,000) kwa kujaribu kuzidisha ugomvi huo na kukosa kuzingatia mahojiano ya usalama ya NBA.

Jokic alitolewa nje zikiwa zimesalia dakika 2:39 kabla ya mchezo kuisha katika ushindi wa 113-96 dhidi ya Miami Heat Jumatatu baada ya kushindwa kujizuia alipochezewa faulo na Morris.

Hali hiyo ilipelekea pacha wa Morris, Marcus kutoa maoni yake kwenye mtandano wa kijamii, Twitter kwamba Jokic alimgonga Markieff kutoka nyuma. Hilo lilipelekea kaka zake Jokic kumwambia Marcus kwenye tweet kujiepushe na ugomvi huo.

Hata hivyo Jokic alitolewa nje ya mchezo akiwa na pointi 25, ribaundi 15 na asisti 10, na sasa Nuggets watawakosa wachezaji wao watatu bora dhidi ya Indiana Pacers ambao ni Jamal Murray ambaye anauguza jeraha la mguu, na Michael Porter Jr. bado yuko nje kutokana na jeraha la mgongo.  

Chanzo: eatv.tv