Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lebron James atangazwa kuwa Bilionea wa kwanza NBA

Le Bron James Billionaire Mcheza Kikapu wa Lakers

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jarida la Forbes, limemtaja mchezaji wa kikapu, LeBron James kuwa bilionea kwa mujibu wa hesabu za jarida hilo.

LeBron anakuwa mchezaji wa kwanza wa NBA, ambaye bado anaendelea kucheza kikapu huku akiwa amefikisha utajiri huo wa zaidi ya Dola Bilioni Moja.

James alikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuwa Bilionea kwani mwaka 2014 alipohojiwa na GQ alinukuliwa akisema:

“Ni adhima yangu kubwa, kiukweli nataka kukuza biashara zangu. Na kama itatokea nikapata, kama nikiwa Bilionea mwanamichezo, mungu wangu! Ntajisikia faraja sana.”

Mcheza Kikapu wa zamani Michael Jordan alikuwa bilionea baada ya kustaafu mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live